Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo mafupi na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio
Colao katika Hoteli ya Sheraton Waldhuus, Mjini Davos, Uswisi,
Viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani unaofanyika mjini
Davos na mazungumzo yao yaliangaza dhamira ya Vodafone ya kuongeza uwekezaji
katika kusaidia ustawi wa jamii nchini na kuunga mkono juhudi za serikali ya
Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo
mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao mjini Davos,
Uswisi.
Vodafone ndio wanahisa wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania.
Bw Colao ambae anahudhuria mkutano wa Uchumi wa Ulimwengu – WEF
mjini Davos kama ilivyo kwa Rais Kikwete walipata nafasi ya kukutana na kufanya
mazungumzo hayo katika hoteli ya Sheraton Waldhuus.
Mazungumzo hayo yaligusia mahusiano ya Vodafone na serikali ya
Tanzania na watu wake hususani katika uwekezaji katika jamii kusaidia
kukuza,kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii nchini ikiwa ni utekelezaji wa
azma na malengo makuu ya Vodafone ya kuchangia kubadili maisha ya watanzania.
Vodafone kupitia Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kiasi
kikubwa cha fedha kusaidia na kuunga mkono miradi mbalimbali ya kijamii nchini
ikiwemo maeneo makuu matano ya Elimu, Afya, Kuinua vipato vya wanawake,
Mazingira na Michezo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo
Katika mazungumzo hayo mafupi Bw. Colao alimuhakikishia Rais
Kikwete kwamba Vodafone itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii Tanzania
hususani katika maeneo ya afya na elimu ambayo yana uhusiano wa moja kwa moja
na wa karibu katika kuiwezesha jamii kuondokana na changamoto ambazo zinaweza
kuathiri maendeleo ya watu na hivyo kushindwa au kupunguza kasi ya kubadili
maisha yao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)