Rais
Dk. Jakaya Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Regia Mtema
aliyekuwa mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoani Morogoro, Regia
Mtema amezikwa Ifakara mkoani humo leo huku mazishi yake yakihudhuriwa
na viongozi wa Serikali na Bunge pamoja na wanasiasa na ndugu jamaa na
marafiki hii leo huko Ifakara, Marehemu Regia alifariki kwa ajali ya
gari iliyotokea Ruvu mkoani Pwani siku ya jumapili.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Regia Mtema aliyezikwa leo Ifakara mkoani Morogoro.
Rais
Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi wa Bunge, Serikali
na Vyama vya siasa wakati alipoongoza wananchi katika mazishi ya
Marehemu Regia Mtema huko Ifakara Mkoani Morogoro kutoka kulia ni Hawa
Ghasia Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Job
Ndugai Naibu Spika wa Bunge, Spika wa bunge Anne Makinda na kutoka
kushoto ni Zitto Kabwe Mbunge wa Chadema Kigoma Kaskazini, Freeman Mbowe
mwenyekiti wa CHADEMA na Joel Bendera Mkuu wa mkoa wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)