Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Martin Manyanya (MB)
--
KIBALI CHA KUUZA MAHINDI NJE YA MKOA WA RUKWA
MKUU WA MKOA WA RUKWA ANAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MKOA UMERUHUSIWA KUUZA MAHINDI NJE YA MKOA NA NJE YA NCHI.
VIBALI VYA KUUZA MAHINDI HAYO VINATOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA BAADA YA KUTIMIZA VIGEZO AU MASHARTI YAFUATAYO:-
1. MAHINDI
HAYO YATAKAGULIWA NA MAAFISA KILIMO TOKA WILAYA HUSIKA NA OFISI YA
MKOA ILI KUONA KAMA YANAKIDHI VIWANGO VYA KUSAFIRISHA KWENDA NJE YA
NCHI NA PIA KURATIBIWA.
2. UTHIBITISHO WA KUWEKWA DAWA YA KUUA WADUDU (FUMMIGATION CERTIFICATE) NA MTAALAM ANAYETAMBULIKA NA SERIKALI.
3. BEI ELEKEZI: BEI YA KUNUNUA MAHINDI TOKA KWA WAKULIMA NI SHILINGI MIA TATU HAMSINI (350/=) KWA KILO AU ZAIDI.
4. MUOMBAJI
WA KIBALI LAZIMA AWE NA LESENI YA BIASHARA. KAMA MASHARTI HAYO YOTE
YATATIMIZWA KIBALI KITAPATIKANA NDANI YA WIKI MOJA.
TAFADHALI ZINGATIA TARATIBU HIZO ILI KUEPUKA USUMBUFU USIO WA LAZIMA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
ENG. STELLA MARTIN MANYANYA (MB)
MKUU WA MKOA WA RUKWA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)