Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri
wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto) leo katika ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es
Salaam. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MKUU
wa mkoa wa Dares Salaam Said Mecky Sadick amesema bado misaada zaidi
inahitajika ili kuweza kuwasaidia wahanga wa mafuriko hususan ya
shughuli za ujenzi na mahitaji ya watoto walioanza shule.
Kauli
hiyo ilitolewa leo (jana) na Sadick wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisi kwake jijini Dares Salaam mara baada ya kupokea msaada
wa hundi ya sh. milioni tano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga
Tanzania, ambayo ilikadhiwa kwake na Mkurugenzi Mkuu Fadhili Manongi.
“Bado
misaada inahitajika tunaendelea kutoa wito kwa watu walioguswa kuweza
kutoa michango yao ili kuweza kusaidia shughuli za ujenzi na mahitaji
ya wanafunzi walianza shule mfano madaftari, vitabu na huduma zingine
zinazohusiana na elimu,” alisema.
Aliongeza
kuwa changamoto nyingine iliyopo ni kujenga nyumba za walimu na
kliniki ya wakinamama na watoto,hivyo aliwaomba Watanzania, taasisi,
mashirika na watu binafsi walioguswa kuendelea kuchangia.
Wakati
huohuo, Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania
(CBCT),kilikabidhi hundi kivuli yenye thamani sh. milioni 10 ya
michango ya vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga hao kwa Mkuu huyo,
ambayo ilikabidhiwa katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina kwa Makamu
wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal jana usiku.
Hundi
hiyo ilikabidhiwa kwa Sadick na Mwenyekiti wa CBRT Zhu Jinfeng,
ambapo alisema misaada mingine imendelea kutolewa hivyo michango hiyo
hadi leo(jana) imefikia sh. milioni 12,550,000.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema agizo la kuangalia uwezekano
wa kuwapatia viwanja wapangaji liko palepale na watalitekeleza kama
alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete, hivyo utaratibu utaanza mara baada
kukamilisha zoezi la wamiliki.
Aliongeza
kuwa utaratibu huo wa wapangaji pia unahitaji fedha kwa ajili ya
kufanya tathimni mpya utoaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha maeneo
hayo.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)