Baadhi ya maada zilizowasilishwa leo katika mkutano wa 21 wa maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akifurahia jambo na Spika wa
Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda baada ya kuhudhuria mada mojawapo
katika mkutano wa 21 wa maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola
unaofanyika Mjini Port of Spain, katika Visiwa vya Trinidad and Tobago.
Spika
wa Ushelisheli na Mwenyekiti wa CPA kanda ya Afrika akisisitiza jambo
katika mkutano wa 21 wa Maspika wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola unaofanyika mjini Port of Spain, Trinidad and Tobago. Kulia ni Spika wa Rwanda Mhe. Rose Mukantabama
Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola waendelea na Mkutano wao wa 21, mjini Port of Spain- Trinidad and Tobago Kama
anavyoonekana Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (katikati) akiwa pamoja
na baadhi ya Maspika Mbalimbali kutoka Mabunge ya nchi wananchama wa Jumuiya
ya Madola wakati wa kujadili maada kuhusu nafasi ya Bunge Kuishauri na
kuisimamia Serikali. Maspika wa nchi wananchama wa Jumuiya
ya Madola wanakutana Port of Spain katika Visiwa vya Trinidad and
Tobago kuazia tarehe 7 hadi 12 January, 2012 katika mkutano wao wa 21
kujadili maswala mbalimbali ya kuimarisha mabunge yao.
Mwenyekiti
wa chama cha mabunge nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) , Mhe.
Sir Alan Haselhurst, Mbunge kutoka Uingereza akichangia nae katika
mojawapo ya mada zilizowasilishwa katika mkutano wa 21 wa maspika wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.Picha na Owen Mwandumbya -Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)