Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Peter Kallaghe akiwakaribisha waheshimiwa wabunge.
Mwenyekiti
wa TAWA UK Mariam Kilumanga na mwana libeneke Jestina George wakiwa
katika picha ya pamoja na Mhe. Al-Shaymaa J. Kwegyir .
Afisa
wa Bunge Mrs Justina Shauri, Mhe. Esther Matiku, Mhe. Beatrice
Shelukindo na Mama Balozi Joyce Kallaghe wakiwa wanamsikiliza mhe.
Balozi akitoa ukaribisho.
Mama Balozi awakaribisha Waheshimiwa Wabunge Wanawake Chakula Cha Jioni nyumbani Kwake
Wageni
hao 12 wakiwemo Wabunge 11 na Afisa wa Bunge 1 waliotokea nyumbani
Tanzania na kuja UK kwa Mualiko wa Commonwealth parliamentarians Group
(CPA) walikaribisha chakula cha jioni na Mama Joyce Kallaghe Mke wa
Balozi wa Uingereza akiwa na Viongozi wa Chama cha TA na TAWA nyumbani
kwake Tanzania hao
Wabunge
hao 11 wote wanawake na ambao miongoni mwao ni Viongozi wa wajumbe wa
Tanzania Women Parliamentarians Group (TWPG) ,waliongozwa na Mwenyekiti
wa TWPG Mheshimiwa Mama Anna Abdalla MP, na wakiwemo Mh.Susan Lyimo MP,
Mh. Magdalena h. Sakaya (MP) , Mh. Angela Kairuki (MP), Mh. Esther
matiko (MP, Mh. Beatrice Shelukindo (MP), Mh. Riziki Omari Juma (MP),
Mh. Namalek Sokoine (MP), Mh . Faharia Hamisi (MP) ,Mh. Al-Shaymaa J.
Kwegyir (MP), Mh. Agripina Z Buyogera (MP) na Afisa wa Bunge Mrs
Justina Shauri.
Wageni
walikaribishwa na Balozi Mheshimiwa Peter Kallaghe na Mama Balozi Joyce
Kallaghe , Mheshimiwa Balozi aliongea machache ya Ukaribisho na kumpa
nafasi Mh.Mama Anna Abdalla ambae alishukuru kwa mualiko huo na
kuelezea kuhusu Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) ambao kila Mbunge
Mwanamke wa Bunge la Tanzania ni mwanachama wake na jinsi gani
TWPG inavyofanya kazi kwa pamoja bila ya kujali itikadi za vyama vya
kisiasa vya Waheshimiwa hao.
Usiku
huo iliweza dhihirika kwa jinsi waheshiwa hao walivyokuja
kujitambulisha kila mmoja alisimama na kujitambulisha na walilotilia
msingi katika utambulisho wao ni kamati zao tofauti za Bunge ambazo
wanahusika nazo na kuwa wnachama wa kikundi cha TWPG. Wageni waliokuwa
pale walishuhudia zaidi ya nusu ya hawa wabunge waliongia na furaha
bila ya kujali kuwa bado wana uchovu wa safari kutoka nyumbani
wakisahau kutaja vyama vyao vya kisiasa. Mheshimiwa Mama Anna Abdalla
alisisitiza kwamba ingawa vyama vya siasa ndio vilivyowapeleka wote
bungeni lakini wakishaingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano
,wanawake bungeni hawaangalii vyama vyao vya siasa bali huwa wakiwa
Bungeni kabla ya sera yeyote kupita Wanawake huwa wote kwa Umoja
wanaangalia hii itamnufaisha vipi Mwanamke na Mtoto wa Kitanzania.
Maneno
haya ya Mheshimiwa Mama Abdalla yalidhihirishwa na jinsi Waheshiwa wote
walipokaa katika meza moja na kuongea na kucheka kwa pamoja na kwa
furaha huku wakila chakula kitamu cha jioni bila ya kujali pale kwenye
ile meza kuna CCM, NCCR, CUF wala CHADEMA. Kitendo hiki kiliwavutia
sana viongozi wa wanawake London ambao walikuwepo katika shuguli
hii Bi. Nelly Msemwa (TA Taifa Deputy chair anaeshughulikia mambo ya
wanwake ),Bi. Mariam Kilumanga(TAWA Chair ), BI Mariam Mungula (TAWA
Secretary) , Bi Rose Kiondo (Afisa Ubalozi) na Bi Jestina George (TA
London na Blogger), kiasi ambacho walipopewa nafasi ya kuongeza
machache walimpa nafasi hii Bi Mariam Mungula ambae aliwashukuru sana
Waheshimiwa Wabunge wa kitendo hicho na somo walilompa la kuwa hata
Wakiwa Bungeni yeye akifikiri hakuna mashirikiano kati ya vyama tofauti
kumbe sivyo kabisa wakiwa ndani na nje ya Bunge wanaweka wote ni kitu
kimoja.
BI
Mariam Mungula vilevile alielezea kaazi za kikundi wa kina mama cha
hapa UK ambacho yeye ni mmjoa wa viongozi wake Tanzania Women
Association (TAWA) na kumalizia kwa kuwaomba waheshimiwa wabunge
kupitia TWPG wasihau kuwa kuna wanawake wengine wa kitanzania hata kama
ni nje ya nchi na ambao wako tayari kushirikiana nao kwa lolote katika
kumuendeleza MWanamke wa KItanzania.
Kikundi
hichi cha Waheshimwa kimekuja Uingereza kwa Mualiko wa CPA kwa siku
chache katika majukumu yao ya kila siku ya kumpingania Mtanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)