MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATUA LUSHOTO JIONI HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATUA LUSHOTO JIONI HII

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jioni hii amemaliza ziara yake katika Wilaya ya Korogwe na kutua Wilaya ya Lushoto tayari kwa kuanza ziara yake katika wilaya hiyo hapo kesho.
 Hawa ni baadhi ya vijana wa lushoto wakiwa pembezoni mwa barabara inayopandisha kwenda lushoto mjini, wakiwa na 'mzigo' maembe wanayosubiri kuyapakia katika magunia na kuuza kwa wafanyabiashara wanaosafirisha kupeleka jijini Dar es Salaam.
 Mzigo wa Kabichi ukisubiri kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam, hapa ni katika Kituo cha mabasi cha Soni, Lushoto.
 Wanafunzi wa shule za msingi wakirejea makwao wakati wakitokea shuleni huku wakiwa na vifaa mbalimbali wanavyotumia kufanyia usafi shuleni.
Hawa nao wakiwa na ndoo, ambapo haikuweza kufahamika mara moja sababu kubwa ya kila mwanafunzi kuwa na ndoo ndogo ya maji wakati akienda shuleni ama kurejea nyumbani, lakini inaonekana ni sababu ya tatizo la maji ambapo waalimu huwaagiza wanafunzi kufika shuleni na maji na pindi wanaporejea makwao pia hupitia maji ya kurudi nayo kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages