Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia
ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye eneo la mradi wa maji wa Chiumbati
Miembeni, wakati alipotembelea mradi huo wa Nachingwea Masasi, akiwa katika
ziara yake ya Mkoa wa Lindi, jana Januari 20, 2012
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa maji wa Chiumbati, Francis
Fumbuka, wakati alipotembelea mradi huo unaoendelea na ujenzi Nachingwe akiwa
katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi, iliyoanza jana Januari 20, 2012. Kushoto ni
mkewe, Mama Zakhia Bilal
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea kadi ya uanachama kutoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya
ya Nachingwea, Hassan Mkope, aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na
CCM, wakati Makamu alipotembelea mradi wa maji wa Chiumbati Nachingwea, akiwa
katika zaiara yake ya mkoa wa Lindi, jana januari 20, 2012
Makamu wa
Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya
kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya
ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara
yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Profesa Mtopea, akizungumza kutoa shukrani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na wananchi wa Nachingwea, wakati alipokuwa akiondoka katika mradi wa
maji wa Chiumbati jana, januari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)