JERRY YANG: MWASISI WA MTANDAO WA YAHOO! AJITOA KWENYE BODI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JERRY YANG: MWASISI WA MTANDAO WA YAHOO! AJITOA KWENYE BODI

Jerry Yang.

JERRY YANG, aliyeasisi mtandao wa Yahoo! mwaka 1955 na David Filo na akawa mtendaji wake mkuu kutoka Juni 2007 hadi Januari 2009, amejiuzulu katika bodi ya kampuni hiyo.

Hatua hiyo ameichukua wiki mbili baada ya kampuni hiyo kumwajiri mkuu wa zamani wa kampuni ya PayPal, Scott Thomshon, kuwa mtendaji wake mkuu mpya.


Yang, ambaye ni raia wa Taiwan, aliwaudhi baadhi ya wana hisa kwa kukataa dau la Dola bilioni 47.5 kutoka kampuni ya Microsoft mwaka 2008 la kuichukua kampuni hiyo. Thamani ya sasa ya kampuni hiyo kulingana na soko ni kiasi cha Dola bilioni 20.


Yang amejiuzulu pia kutoka katika bodi za Yahoo! Japan na Alibaba Group na katika taarifa aliyoitoa alisema: “Wakati umefika kwangu kufuatilia mambo mengine nje ya kampuni ya Yahoo!”
Mkuu huyo wa zamani alielezea pia msimamo wake wa kuunga mkono uongozi wa sasa wa kampuni hiyo ambayo makao yake makuu yako California, Marekani.


“Nimefurahia  kuteuliwa kwa Scott Thomspon kama mtendaji mkuu wa kampuni  kutokana na uwezo wake, na ninaunga mkono uongozi wote wa Yahoo! katika jitihada zake za kuleta mafanikio zaidi,” alisema.
Baadhi ya wachunguzi wa mambo walikuwa wakimwona Yang kuwa kiwazo katika mauzo na kuundwa upya kwa kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages