---
Mwendesha bodaboda ameibuka mshindi wa
milioni 50 za promosheni ya Mzuka wa Airtel, promosheni inayoendeshwa na
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Airtel imemzawadia mshindi wa
droo ya kwanza ya promosheni ya Mzuka wa Airtel milioni 50 katika droo
iliyochezwa wiki iliyopita kisha mwendesha bodaboda bwana Simon Bernard
Simo Mkazi wa Mkuranga aliibuka kuwa mshindi wa promosheni hiyo
iliyoanza mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.
Akiongea wakati wa kusaini fomu ya malipo yake mwendesha bodaboda huyo Bwana Simon Bernard Simo alisema amefurahi kuwa mshindi wa milioni 50, na kwamba hakuamini kuchaguliwa kuwa mshindi. Bw. Simon ambaye pia mbali ya kuwa mwendesha bodaboda anafanya biashara zingine ikiwemo kuuza mafuta ya petroli na kuonyesha mpira wa ligi ya England katika eneo analoishi huko Mkuranga, “nimefarijika kupata kitita hiki cha milioni 50 ambazo nitazitumia katika kupanua na kuendeleza biashara zangu ili kuweza kuongeza mapato na kuweza kusaidia familia yangu” alisema Bw. Simon Berard mshindi wa milioni 50 za Mzuka wa Airtel.
Aidha mama wa mshindi huyo Regina Simon alisema hakuwai kutegemea kuwa mwanae anaweza kuja kupata bahati ya kumiliki mamilioni ya fedha na kudai ana imani Simon akishapata fedha hizo zitawasaidia familia na kuinua hali ya maisha yao.
Akionge kwa niaba ya Airtel Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando alisema “ni kwa mara ya kwanza kampuni yetu ya Airtel tumeamua kuchukua uamuzi wakumtembelea mshindi huyu nyumbani kwake kwani tangu tulipompa amekuwa akionyesha hali ya kutoamini kwamba anaweza kuibuka mshindi wa mamilioni haya kwa hali hii tumeamua kuanzia sasa tutakuwa tukiwatembelea wateja wetu ambao ni washindi wa zawadi kubwa za promosheni zetu ili kila mtanzania aamini juu ya ushindi wao na pia kuwashauri watumie zawadi zao vizuri ili kufaidika kuwa familia ya Airtel ambayo kwa sasa imekuwa na kufikia wateja milioni 50 Afrika nzima ”Tunachukua nafasi hii kuwakumbusha wateja wetu ambao bado hawajajiunga promosheni ya MZUKA ambayo ni bure kufanya hivyo na kuweza kupata nafasi ya kuibuka kuwa washindi wa zawadi mbalimbali zikiwemo Simu za mkononi aina ya Samsung, muda wa maongezi au pesa taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 50 kila mwisho wa mwezi" Aliongeza Mmbando.
Promosheni ya Mzuka wa Airtel inaendelea mpaka mwishoni mwa mwezi wa pili, wateja wetu wote wajiunge na kushiriki ni rahisi kujiunga na ni bure tuma neno Mzuka kwenda namba 15565 na uwe mmoja kati ya washindi wa zawadi mbalimbali, kadri unavyo recharge na kutumia simu yako ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda zaidi

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)