WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi
ameitaka kamati maalum ya kupendekeza Vazi la Taifa kutimiza wajibu wake
ipasavyo ili kukamilisha mchakato huo kwa muda uliokusudiwa.
Waziri Nchimbi alisema hayo leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,
wakati alipoizindua rasmi kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti
Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga.
“Napenda niwaaeleze wananchi kwamba sikukurupuka kuteua wajumbe wa
kamati hii, nilipata ushauri toka kwa watu mbalimbali.Wajumbe mnayokazi
kubwa sana kwani ni lazima tufike mwisho na tuwape Watnaznia kile
ambacho wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu na baada ya kupatikana vazi
mtasaisdia kulitangaza ili wananchi walijue,”Aliongeza.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kusaga pamoja na kushukuru kwa kuteuliwa
huko, alisema kamati yake itafanya kazi hiyo kwa nguvu zote kuhakikisha
vazi hilo linapatikana.
Mbali na Kusaga kamati hiyo inaundwa pia na Angela Ngowi (Katibu),
Habibu Gunze, Bibi.Joyce Mhaville, Bw.Mustafa, Hassanali, Absaloom
Kibanda, Makwaiya Kuhenga na Ndesambuka Merinyo ambao ni Wajumbe
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)