Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Bia ya Serengeti (SBL) imeahidi kuendelea kudhamini mashindano
mbalimbali ya gofu katika ngazi mbalimbali ikiwa ni mkakati wa kampuni
hiyo wa kuundeleza mchezo huo.
Meneja
wa Tusker, Rita Mchaki alisema wakati wa mashindano ya ‘Tusker Malt
Waitara Trophy’ yaliyofanyika katika viwanja vya Lugalo mwishoni mwa
wiki kuwa kampuni hiyo imepanga kuweka bajeti endelevu katika udhamini
wa mchezo huo kila mwaka.
Mashindano
hayo ambayo yatafanyika kila mwaka yalidhaminiwa na SBL kupitia
kinywaji chake cha Tusker Malt kwa thamani ya milioni kumi ambapo timu
za kada mbalimbali ikiwemo wachezaji waalikwa kutoka nchi jirani
walishiriki.
Alisema
SBL imekuwa na mchango mkubwa katika michezo hususani upande wa mpira
wa miguu na kwamba sasa inapanga kuwekeza katika michezo mingine ili
ushiriki wa Tanzania katika michezo ya kimataifa uwe katika wigo mpana.
“Tumewezesha
kufanyika kwa mashindano haya lakini hatutaishi hapa tutafanya hivi
kila mwaka kulingana na uwezo wetu kifedha na sasa SBL ina mipango ya
kupanua wigo wa kuwekeza katika michezo ili ushiriki wa Tanzania katika
michezo ya kimataifa iwe katika wigo mkubwa,” alisema Mchaki.
Pamoja
na mashindano hayo SBL pia imedhamini mashindano makubwa mawili ya gofu
mwezi Novemba mwaka huu ya Gofu ya Afrika Mashariki 2011 yaliyoisha
hivi karibuni katika viwanja vya Gynkhana Arusha.
Katika
mchuano huo Salehe Yahaya aliibuka mshindi kwa upande wa vijana akipata
jumla ya mirejesho 71 akiwabwaga wapinzani wake Kadio Hassan na Braison
Nyenza waliopata mirejesho 75 na 77.
Katika
kundi la wachezaji wa rika la juu kombe lilienda kwa Brigedia Generali
mstaafu Julius Mbilinyi aliyepata mirejesho 70 akimbwaga Simon Sayore na
Mkuu wa Jeshi Mstaafu George Waitara walioshika nafasi za pili na tatu
kwa mirejesho 73 kwa 78.
Kwa
upande wa wanawake, kikombe Hawa Wanyeche alipata mirejesho78 na Angel
Eaton aliyechukua nafasi ya pili alipata 81 na Fatuma Makame alishika
nafasi ya tatu kwa jumla ya mirejesho 82.
SBL
ilitoa zawadi zaz fedha taslimu kwa viwango tofauti kwa wachezaji wote
pamoja na zawadi mbalimbali za promosheni ikiwa kama changamoto kwa
washiriki hao kufanya vizuri katika mshindano yajayo mwakani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)