Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa
hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana
Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo
Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa
ukumbini wakati akisubiri kuapishwa rasmi kushika madaraka ya Katibu
Mkuu Kiongozi badala ya Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon
Luhanjo (kushoto) akimkabidhi nyaraka za serikali maalum kwa kuapishiwa
na Biblia, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ili
kuanza kuapishwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salam leo
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi,
Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu
Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla
hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa
pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon
Luhanjo, akisimamia zoezi hilo
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Nyaraka
za Serikali, Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Ombeni Yohana Sefue, mara
baada ya kumuapisha rasmi, leo Ikulu Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana
Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa
katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana
Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo
baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es
Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni
Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu,
Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu
kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi
mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu
wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi
iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon
Luhanjo, akihojiwa na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa
hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana
Sefue Ikulu Dr es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)