MSONDO NGOMA YAFANYA SHOW SAFI NDANI YA UKUMBI WA TCC CHANG'OMBE USIKU WA KUAMKIA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MSONDO NGOMA YAFANYA SHOW SAFI NDANI YA UKUMBI WA TCC CHANG'OMBE USIKU WA KUAMKIA LEO

Wanamuziki Shaban Dede na TX Moshi William Junior wa Msondo wakiimba jukwaani huku mashabiki wakiwashangilia kwelikweli wakati wa onyesho hilo lililofanyika TCC Chang'ombe usiku wa kuamkia leo. 
Kutoka kulia ni mwimbaji wa Bendi ya Sikinde Hassan Kunyata, Yusuph Bernald na Shaban Lendi wapiga Saxaphone wakifanya vitu vyao jukwaani. 
Umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria katika onyesho hilo usiku wa kuamkia leo. 

Mwanamuziki chipukizi mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Msondo TX Moshi William TX Moshi William Junior, akinyanyuliwa juu juu na mashabiki wa bendi hiyo wakati alipokuwa akiimba katika mpambano wa bendi za Msondo Band na DDC Mlimani Park Sikinde jana, kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam.
Mpambano huo ulivuta mashabiki wengi katika viwanja vya TCC Sigara ambapo bendi ya Msondo, ilionekana kuwapiku wenzao wa Sikinde kutokana na Shamrashamra zilizokuwa zikitawala wakati Msondo wakiimba jukwaani, Onyesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo ikiwa ni pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismas.Picha na John Bukuku.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages