Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera , akihutubia wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la Bima ya Afya, la kwanza la Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, lililofanyika mjini Morogoro jana.
Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Khamis Mdee, akifafanunua mambo mbalimbali yahusuyo mfuko huo wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Emmanuel Humba (kulia),
akiwaeleza waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), umuhimu wa
kuuboresha mfuko huo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho, wakati wa
kongamano la kwanza la waratibu wa mfuko huo nchini, lililofanyika
kwenye Hoteli ya Kisasa ya Nashera, mjini Morogoro, jana.
Baadhi
ya Waratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) nchini, wakishiriki katika
kongamano la kwanza la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali ya
kuboresha huduma za mfuko huo, lililofunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, Joel Bendera, mjini Morogoro jana.
Moja ya makundi ya Waratibu wa CHF, wakijadiliana jinsi ya kuweka mikakati ya uboreshaji wa mfuko huo.Picha na Richard Mwaikenda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)