VODACOM TANZANIA, CLOUDS FM,SERENGETI BREWERIES ZANYAKUA TUZO YA SUPER BRAND HYATT REGENCY USIKU WA LEO JIJINI DAR ES SALAAM - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM TANZANIA, CLOUDS FM,SERENGETI BREWERIES ZANYAKUA TUZO YA SUPER BRAND HYATT REGENCY USIKU WA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akimkabidhi tuzo ya Superbrandy Bw. Joseph Kusaga mkurugenzi wa Clouds Fm , katikati ni Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrandy East Africa Jawad Jaffer, katika hafla ya kutoa tuzo kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika ubora wa viwango vya bidhaa na kukubalika kwa walaji, katika hafla inayofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam usiku huu, ambapo makampuni mbalimbali yatapata tuzo hizo kutoka kwa taasisi hiyo.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akimkabidhi tuzo ya Superbrandy Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo,katikati ni Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrandy East Africa Jawad Jaffer
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akimkabidhi tuzo ya Superbrandy kwa Mwamvita Makamba Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom kushoto, katikati ni Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrandy East Africa Jawad Jaffer na kulia ni Ofisa Bidhaa wa Vodacom Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akisoma hotuba yake katika utoaji wa tuzo hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrandy East Africa Jawad Jaffer naye akizungumza machache kabla ya kutoa tuzo hizo.
Kundi la Wanne Star likitumbuzi katika hafla hiyo
Wageni waa;likwa kutoka makampuni mbalimballi wakiwa katika hafla hiyo
Mkutrugenzi wa Clouds Radio Joseph Kusaga kushoto ni mmoja wa wakurugenzi wa makampuni waliohudhuria katika hfla hiyo.
Kutoka kulia ni Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager, Ephraim Mafuru Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti na kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii Nandi Mwiyombela.
Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Charles Kimei akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo kabla ya utoaji wa tuzo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki akizungumza na Ranjit Babla Mkurugenzi wa kampuni ya TrinstarInvestment Co. Ttd, katikati ni Mkurugenzi wa CRDB Bw. Charles Kimei.
Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mahusiano ya Jamii wa kampuni hiyo Nandi Mwiyombela nao wamehudhuria katika hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki akizungumza na Mwamvita Makamba Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom, kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu kabla ya kuanza rasmi kwa hafla hiyo, kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa
Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Bi Tully Mwambapa kabla ya kuanza kwa hafla hiyo usiku huu. Mwamvita Makamba Ofisa Mkuu wa Masoko na mahusiano wa kampuni ya Vodacom akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda.Picha Zote na John Bukuku Wa Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages