Ghasia zimezuka tena katika Mji
Mkuu wa Misri wakati vikosi vya usalama vinajaribu kuwaondoa
waandamanaji kutoka medani ya Tahrir mjini Cairo. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi wakati
waandamanaji waliokuwa katika medani hiyo wakivurumisha mawe na mabomu
ya kujiundia ya moto. Wizara
ya Afya inasema kuwa watu 20 walikufa siku ya jumapili na kuongeza
idadi ya wote waliokufa kutokana na ghasia hizo kufikia 22 na wengine
1,750 kujeruhiwa tangu ghasia kuanza Jumamosi.
Hatahivyo maafisa wa chumba cha kuhifadhia maiti baadae leo wamesema kuwa idadi ya waliokufa hadi sasa ni watu wasiopungua 33. Waziri wa utamaduni Emad Abu Ghazi amejiuzulu kutokana na ghasia hizo. Mena-shirika rasmi la habari nchini humo
limesema kuwa Waziri huyo amejiuzulu akipinga njia iliyotumiwa na
serikali katika kukabiliana na waandamanaji. Maandamanao haya ndiyo yamechukuwa muda mrefu zaidi tangu yale ya kumpinga Rais Hosni Mubarak mwezi February.
Waandamanaji wanahofu kuwa jeshi huenda linataka kung'ang'ania madaraka. Baraza hilo, linaloongozwa na Field Marshal
Mohamed Tantawi, linajukumu la kusimamia nchi hiyo wakati inaingia
katika demokrasia baada ya miongo mitatu ya utawala wa kimabavu chini ya
Bw. Mubarak.
Waandamanaji walisikika wakimtaka ajiuzulu katika maandamano hayo ya mwishoni mwa wiki. "Wanajeshi waliahidi wataachia madaraka katika
kipindi cha miezi sita" mmoja wa waandamanaji hao alisema."sasa miezi
kumi tayari imeshapita na bado hawajatimiza ahadi zao, tunaona kama
wanatuhadaa"
SOURCE: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)