Vodacom FoundationTanzania Yatoa Msaada Wa Madarasa Mawili Mkoani iringa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Vodacom FoundationTanzania Yatoa Msaada Wa Madarasa Mawili Mkoani iringa

Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya  shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga akiongea na wazazi na wanafunzi wa kata ya Kalenga Mkoani Iringa wakati wa hafla ya kuwakabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 kwa  shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani humo ,yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”Kulia ni Afisa Elimu  wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.
 
Afisa Elimu  wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa akikata utepe kuashiria kupokea msaada  wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya  shilingi Milioni 29 yaliyojengwa na  Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri, iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa, wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya kusini Jackson Kiswaga,Diwani wa kata ya Kalenga Ameria Galinoma na diwani viti maalum Shakila Kiwanga.
 
Mkuu wa mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania  Yessaya Mwakifulefule akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lipuri  iliyopo  kata ya Kalenga mkoani Iringa Agness John,mara baada ya kukabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko huo.Akishuhudia  watatu kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo Alex Mwakiyanga akiwa na walimu wa shule hiyo.
Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu  Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga kwa kumkabidhi mkuki baada ya kumvisha vazi la mgorole ikiwa ni heshima kubwa kwa mkoa huo wakati walipofika kukabidhi  madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni 29 katika shule ya sekondari ya Lipuri mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages