Taswira Za Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa Ya CCM Mjini Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Za Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Taifa Ya CCM Mjini Dodoma


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume,akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa,Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC,katika ukumbi wa white house Mjini Dodoma.
Mjumbe wa NEC na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa ufafanuzi kuhusu jambo lililokuwa likijadiliwa katika kikao hicho .
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa na Waziri Ali Juma Shamuhuna mjumbe wa NEC,wakibadilishana mawazo wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa huko Dodoma.
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania,pia mjumbe wa Mkutano wa Halamashauri Kuu ya CCM Taifa,Mhe Fredric Sumaye,akisalimiana na Katibu wa sektariueti ya Oganization ya CCM Mhe Asha Abdalla Juma,katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma,ukiwa mkutano huo unaendelea kwa siku ya pili jana
Wajumbe wa NEC, Spika wa Bunge Anna Makinda na Abdulrahman Kinana wakitazama jarida la masuala ya siasa wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi CCM, Nape NNauye akifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali iliyokuwa ikiendelea katika mkitano wa NEC mjini Dodoma Jana. Kulia ni Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba.
Katibu wa NEC, Mambo ya Nje Januari Makamba na Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma wakijadili jambo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
Wajumbe wa NEC, Angella Kairuki na Anna Abdallah wakionyeshana mambo kwenye mtandao wakati wakiwa kwenye kikao cha NEC jana
Katibu wa NEC Oganaizesheni Asha Abdallah Juma akimsalimia Mjumbe wa NEC Andrew Chenge.Picha Bashir Nkromo  na Ramadhani Othman Wa Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages