Na Mwandishi Maalumu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Jakaya
Kikwete, Novemba 26, 2011, ametunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika kwenye Chuo cha Kijeshi Monduli, Arusha,
Rais Kikwete ametoa kamisheni kwa maofisa wanafunzi 506 waliofanikiwa
kumaliza mafunzo mafupi ya 27.
Kati ya maofisa hao wanafunzi, 69 ni maofisa wa kike na 437 ni
maofisa wa kiume na maofisa wote ni wanataaluma wakawa ni pamoja na
walimu 101, maofisa mawasiliano ya umma 54, wataalamu wa utawala 48 na
wahasibu 167.
Maofisa wengine walitunukiwa kamisheni katika sherehe za leo ni
wataalam wa kilimo 14, wahandisi tisa, wanasheria 52, wanahistoria na
utamaduni 12, waandishi wa habari 43, wataalam wa ugavi watatu na
waataalam wa sayansi ya mazingira watatu.
Wakati huo huo, Rais Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Waziri
Mkuu wa Kenya, Mheshimiwa Raila Odinga. Viongozi hao wawili wamekutana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wakati Rais
Kikwete akirejea Dar es Salaam jioni.
Viongozi hao wamezungumzia masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano
kati ya Tanzania na Kenya na yale ya kikanda.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)