PAMOJA NA TAIFA STARS KUCHAPWA GOLI NA CHAD YAFUZU HATUA YA MAKUNDI KWA GOLI LA UGENINI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

PAMOJA NA TAIFA STARS KUCHAPWA GOLI NA CHAD YAFUZU HATUA YA MAKUNDI KWA GOLI LA UGENINI


 Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars, Jan Poulsen, akiwa hoi akishika kiuno baada ya mpira kumalizika na timu yake kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Chad katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Mbwana Samatta, akimtoka beki wa Chad, Sylvain Doubam, wakati wa mchezo marudiano kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mpaka hivi sasa bado ni droo na mpira ni mapumziko ukitarajiwa kuanza kipindi cha pili baada ya dakika chache zijazo.
Kiungo Mshambuliaji wa Stars, Nizar Khalfan, akijiandaa kupiga kona wakati wa mchezo huo.
Chad 1, Stars 0, Mrisho Ngasa, akimtesa beki wa Chad.
Kwa matokeo hayo sasa timu ya Taifa Stars imefanikiwa kupenya katika  michuano hiyo ya hatua ya awali ya mtoano kutinga kwenye makundi ya kushiriki katika kundi C lenye jumla ya timu nne za Ivory Coast, Morocco na Gambia, kuelekea fainali za Kombe la Dunia zinazotarajia kufanyika 2014 nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages