KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE LEO MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE LEO MJINI DODOMA

Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi akibadilishana mawazo na Mbunge wa Nkenge (CCM) Bi. Asumpter Mshama nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu. 
Katibu Mtendaji wa shirikisho la filamu Tanzania, Wilson Makubi akitoa mada katika semina elekezi kwa Maafisa utamduni wa Halmashauri mbalimbali za wilaya nchini juu ya matumizi ya kanuni mpya za filamu na michezo ya kuigiza. Semina ya siku mbili itafanyika katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma na inatarajia kufungwa rasmi kesho tarehe 19/11/2011.
Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Patrick Kipangula akitoa ufafanuzi kwa Maafisa Utamaduni kuhusu vifungu vya kisheria vya kanuni mpya za filamu na michezo ya kuigiza vilivyo wakati wa semina elekezi kwa maafisa hao inayofanyika katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma. Semina hiyoinatarajia kufungwa kesho tarehe 19/11/2011.
Mbunge wa Mafia (CCM)Abdulkarim Shah akizungumza na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani vya NCCR mageuzi na CHADEMA nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi) David Kafulila anayefuatia ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema) Ezekia Wenje na katikati ni Mbunge wa Ksulu Mjini (NCCR Mageuzi), Moses Machali .Picha na Anna Itenda- Maelezo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages