Mzee Asumwisye
Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), akiwa hoi jana siku ya
jumapili baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha
Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za
kishirikina.
Mkuu wa kituo cha polisi cha
Iyunga(kushoto) na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikuti Bwana Emanuel
Mwasote(katikati mwenye shati ya pink) wakijaribu kuokoa maisha ya Mzee
Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), kwa kumpeleka
Kituo cha polisi Iyunga, baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia
kwenye nyumba yake na kutaka kuichoma moto jana siku ya jumapili kabla
ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya
Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Hata hivyo juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya wananchi hao kuwazidi
nguvu polisi kutokana na Jeshi la polisi kushindwa kufika mapema eneo
la tukio na kuaanza kumdondoshea kichapo.
Bwana Richard Mwakalinga
akijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa
miaka 60(Pichani),wakati wananchi wa kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga
jijini hapa kuanza kumdondoshea kichapo jana siku ya
jumapiliwakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina, wakati Jeshi
la polisi halijafika eneo la tukio ili kuwedha kuwadhibiti wananchi
hao.
Wananchi wenye hasira kali
Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya, wakimpiga kwa mawe
Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), hapo jana
siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Hapa ni nyumba ya Mzee Asumwisye
Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kuvunjwa na yeye akiwa
ndani ya nyumba hiyo baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji
alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya
kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali
wakivunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60,
jana siku ya jumapili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji
alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya
kujihusisha na Imani za kishirikina.
Wananchi wa kitongoji alichokuwa
akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimzingira
Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya
kumdondoshea kichapo wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali
wakiendelea kuvunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri
wa miaka 60, jana siku ya jumapili, ambapo akina mama nao hawakukaa
nyumba kushiriki tukio hili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa
kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini
Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
Baada ya kupingwa
Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya
jumapili, Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tukio na
kumchukua mzee huyo na kumpeleka Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini
Mbeya. Pichani ni baadhi ya askali na raia wema wakimuchukua mzee huyo
na kumpeleka kwenye gari la polisi kabla ya kumkimbiza hospitali.
Mke wa Mzee Asumwisye
Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, katikati akilia kwa uchungu na
kupewa msaada na wanawake wenzake, baada ya mumewe kudondoshewa kichapo
kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti, kata ya
Iyunga jijini Mbeya jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na
imani za kishirikina.
HITIMISHO
Maoni ya mtandao
Jeshi la polisi linapaswa kufika kwa wakati muafaka mara baada ya
kupewa taarifa, lakini pia elimu itolewe kwa wananchi kutojichukulia
sheria mikononi kwani tuhuma na sio uthibitisho, kwani mahakama pekee
ndio ina mamlaka ya kutoa hukumu.
Habari Kwa Hisani Ya Mbeya Yetu/(Picha na habari na Ezekiel Kamanga)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)