Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikani Tanzania, Costantino Mokiwa (kushoto),
akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga ambaye
alichangia sh. mil. 3,katika harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa
mabweni ya Shule ya Sekondari ya Askofu John Sepeku iliyopo Buza Mtoni,
Dar es Salaam.
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikani Tanzania, Costantino Mokiwa (kushoto)
akipokea mchango wa sh. mil 10 kutoka kwa mke wa Waziri Mkuu mstaafu,
Edward Lowassa (katikati), Regina Lowassa, zilizotolewa na familia ya
Lowassa katika harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa mabweni ya Shule
ya Sekondari ya Askofu John Sepeku iliyopo Buza Mtoni, Dar es Salaam.
Lowassa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyofanyika
Kanisa la Aglikani Segerea, Dar es Salaam jana,ambapo zaidi ya sh. mil.
126.9 zilichangangwa. Waziri Mkuu mstaafu aliahidi kutoa tena sh.
milioni 10.Picha na Mpiga Picha Wetu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)