Naibu
waziri wa Uchukuzi, Eng. Dkt. Athuman Mfutakamba (Mbunge) akimkabidhi
Bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzaia 2011, Salha Israel, tayari
kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia (Miss World 2011)
yaliyopangwa kufanyika London, Uingereza Novemba 6.
Habari na Picha kwa Hisani ya kitengo cha Habari cha Miss Tanzania.
Mbali
ya kukabidhi bendera, Naibu Waziri pia alimchangia salha Dola 1000 kwa
ajili ya safari hiyo huku wafanyakazi wa wizara yake wakitoa Sh. Milioni
3.4, kwa ajili ya kumchangia mrembo huyo anayekwenda kuiwakilisha nchi
katika mashindano hayo ya Dunia.
Aidha
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kilikabidhi Dola 2000 kwa mrembo
huyo kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Nakuala Senzia.
Senzia
pia alimkabidhi, Salha, kifurushi kinachoelezea vivutio mbalimbali vya
utalii na uwekezaji vya Tanzania ambavyo Salha atavitumia wakati wa
kuinadi nchi akiwa katika kambini ya mashindano hayo. Habari na Picha kwa Hisani ya kitengo cha Habari cha Miss Tanzania.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)