Transforma iliyopo ndani ya uzio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Imeripuka mchana wa leo na kufanya wafanyakazi wa Shirika hilo kukimbia huku wengine wakijaribu kufanya utaratibu wa kuuzima moto uliokuwa ukiwaka kwenye Transfoma hilo.Hii ni mara ya pili kulipuka kwa Transfoma hilo baada ya juzi jumanne kulipuka na kuwahiwa kuzimwa.

Inaelezwa kuwa transfoma hiyo iliyoripuka leo ni mpya baada ya kubadilishwa ile ya awali iliyowaka juzi. wachina wa Star Times ndiyo waliotaharuki zaidi kwani ofisi zao almanusura ziungue kutokana na ukaribu wa na Transfoma hilo.

Baadhi ya ofisi za TBC, ambazo ziko jirani na transforma hilo zimeungua moto.Kikosi cha Zima Moto Kama kawaida yake kilifika eneo la tukio kwa kuchelewa na kukuta baadhi ya sehemu zishaungua kwa moto huo.
Kwa Sasa moto huo ushazimwa na taratibu zingine zinaendelea ili kujua nini chanzo cha kuungua kwa Transfoma hilo. Moto ukiendelea kuwaka kwa kasi.Moshi mzito ulitanda angani wakati Transfoma hilo linawaka.Kwa Hisani Ya Michuzi Blog

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)