TASWIRA MBALIMBALI ZA MKURUGENZI WA VODAFONE ALIPOTEMBELEA TANZANIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA MBALIMBALI ZA MKURUGENZI WA VODAFONE ALIPOTEMBELEA TANZANIA

Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao katikati akimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi wa CCBRT Haika Mawala akiongea mara alipotembelea hospitali hiyo akiwa na lengo la kutoa msaada kwa kina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa festula mara alipowasili nchini hivi karibuni,Kushoto Ofisa Mkuu wa masoko na mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba. 
Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao(kulia)akijadiliana jambo na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Samwel Mwakipesile mara alipowasili nchini  kwa lengo la kujionea jinsi gani kampuni hiyo inavyoendesha  shughuli zake hapa nchini .
Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao akisalimiana na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara alipowasili nchini hivi karibuni akiwa na lengo la kujionea  jinsi Vodacom Tanzania inavyoendesha shughuli zake.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao(kulia)akifafanua jambo kwa baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali za Vodacom Tanzania,alipokuja nchini hivi karibuni kujionea jinsi Vodacom Tanzania inavyoendesha shughuli zake,kutoka kushoto Steven Kingu,Nector Foya,Evancy Limo,Philimon Chacha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wameshikilia bendera ya Taifa kwenye siku ya Vodacom 50 year Independent day na kumpokea Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao,alipokuja nchini  hivi karibuni kujionea jinsi Vodacom Tanzania inavyofanya shughuli zake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages