Morris
Njowoka Meneja wa kinywaji cha Malta Guinness akimkabidhi zawadi mmoja
wa washindi wa wa mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Open Cycle
Challenge.
Mkurugenzi
wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti SBL Ephraim Mafuru akimpongeza
Sophia Husein kutoka klabu ya Arusha Cycling aliyeshinda kilomita 80
wanawake baada ya kupokea zawadi zake kulia ni Moriss Njowoka Meneja wa
kinywaji cha Malta Guiness..
Hatimaye
Richard Laizer wa mkoani wa Arusha ndiye ametegua kitendawili cha nani
anayepaswa kuwa mshindi wa mbio za wazi za baiskeli za Vodacom Mwanza
Open Cycle Challenge baada ya kuwashinda washiriki wengine zaidi ya
400 walijitokeza kushiriki kwenye mashindano hayo kwa upande wa
wanaume.
Hapa mshindi huyo
wa mbio za Mwanza Open Vodacom Cycle Challenge 2011 kutoka klabu ya
Arusha Cycling Richard Laizer akipokea zawadi yake ya shilingi milioni
1.500.000 kutoka kwa Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania
George Rwehumbiza mara baada ya kutajwa katika mbio hizo za kilomita 196
zilizoanzia Busanda mkoani Shinyanga na kumalizikia Bugando Hills
jijini Mwanza. Mbio hizo
ziligawanyika katika makundi matatu ambapo kulikwa na wanawake wenye
ulemavu ambao waliendesha baiskeli kilomita 10 wakati wanaume wenye
ulemavu waliendesha umba;li wa kilomita 15.
Kwa upande mwingine
kulikuwa na mbio za wanawake ambao waliendesha baiskeli kwa umbali wa
kilomita 80 wakati wanaume wakiendesha kwa umbali wa kilomita 196 ambao
ndiyo ulikuwa umali mrefu zaidi
Katika Picha kulia ni Steven Kingu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda
ya Ziwa na kulia kwa George Rwehumbiza ni Mkurugenzi wa Masoko wa
Kampuni ya bia ya Serengeti SBL.
Mdhamini mkuu wa mashiundano hayo ni kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom ikishirikiana na wadhamini wenza kampuni ya bia ya Aerengeti SBL
na Kituo cha redio cha Clouds









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)