Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Amtembelea Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Amtembelea Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,Mkurugenzi wa Vodafone Vitorio Colao, Mkurugenzi wa kimataifa wa maswala ya kibiashara wa Vodacom  Afrika ya kusini Johan Dennelind.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare,ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulienda Ikulu hivi karibuni kujadili maswala  mbalimbali ya kibiashara,wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa kimataifa wa maswala ya kibiashara wa Vodacom Afrika ya kusini Johan Dennelind,Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao,ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulienda Ikulu hivi karibuni kujadili maswala  mbalimbali ya kibiashara,anaeangalia kushoto Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda,kulia Mkurugenzi wa kimataifa wa maswala ya kibiashara wa Vodacom Afrika ya kusini Johan Dennelind.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Meneja wa mfuko wa Vodacom wa kusaidia wakina mama nchini(Mwei)Mwamvua Mlangwa,na Ofisa mkuu wa masoko na mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa   Vodacom Tanzania Dietlof Mare,ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulienda Ikulu hivi karibuni kujadili maswala  mbalimbali ya kibiashara,wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa kimataifa wa maswala ya kibiashara wa Vodacom Afrika ya kusini Johan Dennelind,Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Vitorio Colao.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages