Picha
ya Mhifadhi Olman Walley ikiwa ni kielelezo cha kuonyesha jinsi ya
utamaduni wa vazi la zamani la asili ya watu wa Australia .
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kulia) akiangalia aina mbalimbali za vito
vya madini katika jengo la Perth Council House Perth Australia
Okt.29,2011 wakiwa katika ziara ya wake wa viongozi waliohudhuria
mkutano mkuu wa nchi wanachama wa jumuia ya madola pamoja na Mwenyeji
wake Patner wa waziri mkuu wa Australia Bw, Tim Mathieson (mwenye suti)
katika ziara hiyo wamejifunza umuhimu wa sekta ya nishati na madini kwa
nchi ya Australia.
Mama
Salma Kikwete akionyeshwa vazi la asili-na mhifadhi olman walley- Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiangalia pamoja na kupatiwa
historia mbalimbali kuhusu aina ya vazi liliotengenezwa kwa ngozi ya
mnyama wa asili ya Kangaroo . kutoka kwa mhifadhi Olman Walley
walipotembelea bustani ya mimea ya asili pamoja na wanyama katika eneo
maalumu la King's Park Austaralia.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiwa pamoja na baaadhi ya wake wa
viongozi wawaliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuia
ya madola wakiangalia sanaa ya asili wa watu wa nchi ya Australia
oktoba 29. 2011 inayopigwa na Olman Walley walipofanya ziara ya
kuangalia aina mbalimbali ya wanyama ,bustani ya hifandi ya miti ya
asili kwenye eneo la Caversham Wildlife Park .Pichani wa pili kulia ni
Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)