Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
Tanzania Philipo Mulugo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Songwe lililopo
wilayani Chunya mkoani Mbeya aliyesimama akitoa hotuba katika moja ya
mikutano yake.
Na mwandishi wetu.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mheshimiwa Philipo Mulugo amesema serikali imerejesha mtihani wa taifa wa kidato cha pili ili kupunguza kushuka viwango vya ufaulu hasa kwa kidato cha nne nchini.
Ameyasema hayo wakali alipokuwa akiwahutubia wananchi waliompa dhamana ya ubunge katika jimbo la Songwe, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na kuongeza kuwa wastani wa ufaulu wa mtihani huo utakuwa ni alama 25.
Amesisitiza kwa kusema kwamba kuanzia mwaka huu hakuna mwanafunzi ambaye ataruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu kama hatukuwa amefanya mtihani wa kidato cha pili na kupata alama zilizowekwa.
Taarifa tulizozipata zinadai kuwa wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani yao ya kidato cha nne ndio hao ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitiyani yao ya kidato cha pili

Wakati huo huo mheshimiwa Mulugo
amesema wananchi waliokosa elimu ya Sekondari wametangaziwa neema ya
kusoma bure elimu ya Sekondari Jimboni humo.
Mulugo alisema
kuwa kwa kuanzia tayari anasomesha wananchi 20 jambo ambalo alisema
kuwa linamuumiza kwani yupo tayari kuwalipia wananchi wote wenye
uhitaji wa elimu hiyo ya Sekondari ambapo anatarajia kuanzisha Maktaba
ya Jimbo ambayo itakuwa eneo la Mkwajuni.
Alisema kuwa Jimbo
hilo la Songwe na wilaya nzima ya Chunya ni moja ya wilaya ambazo zipo
nyuma sana kielimu jambo ambalo viongozi wanaopata fursa akiwemo yeye
ni lazima wafanya jitihada za kuwasaidia wenye uhitaji.
Naibu Waziri huyo
wa elimu maarufu kama Mulugo Ahadi umepata, aliongeza kuwa kufikia
mwakani 2012 atafarijika endapo wananchi hao watajitokeza kujiunga na
vituo hivyo vinavyotoa mafunzo ya elimu ya Sekondari kwasababu
ulimwengu uliopo sasa unahitaji wasomi ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazoukabili.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)