------
TUKIO la burudani la Dar es Salaam
Quiznite lililofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki lilifana kwa
kiasi kikubwa ambapo burudani ya muziki na sarakasi ziliteka mashabiki
waliofika katika tukio hilo.
Pamoja
na burudani tukio hilo lilihusisha mashindano ya kujibu maswali
katika nyanja za muziki, michezo,elimu ya uraia na filamu ambapo
washiriki waliunda makundi ya watu kumi kumi yalioingia katika
mchuano.
Katika
mchuano huo kundi la Mwananchi liliibuka washindi na kujinyakulia
fedha taslimu sh. mil 1/= na kundi lililojiita Synovate liliibuka kuwa
washindi wa pili na kundi la Chondechonde lilishika nafasi ya tatu na
kujinyakulia zawadi kutoka kwa wadhamini.
Meneja
wa kinywaji cha Tusker Malt waliodhamini tukio hilo alisema kampuni
yake imefarijika na muitikio wa watu katika tukio hilo ambalo ni jipya
katika jamii ya kitanzania.
Alisema
Dar es Salaam Quiznite imetokana na tukio la kidunia linalojulikana
kama Quiznite World linalofanyika katika nchi mbalimbali likiwa na
lengo la kuwakutanisha watu wa rika mbalimbali na nyanja tofauti
katika kubadilishana mawazo.
“Hii
ilikuwa nafasi nyingine kwa wanywaji wetu kupata wigo mpana wa kuwa
karibu na kinywaji cha Tusker Malt katika burudani ambayo itawasaidia
kujenga mahusiano baina yao na marafiki zao ndani ya sekta tofauti”,
alisema Mchaki.
Kwa upande wake Meneja wa Quiznite World Vincent Adour alisema anaamini uwanja huo wa majadiliano ni
nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwa wengine ikiwa ni pamoja na
kupanua wigo wa kufahamiana na wakati fulani kupanua soko la biashara.
Alisema
tukio hilo sasa litakuwa linafanyika Tanzania katika kipindi cha kila
robo mwaka na kwamba wanaamini tukio litakalofuata litakuwa kubwa
zaidi na kuwavutia wengi kushiriki.
"Dar
es Salaam Quiznite imefungua milango kwa matukio mengine
yatakayofuata kwani tunaamini matukio yatakayofuata yatakuwa na wigo
mpana zaidi wa ushiriki," alisema Adour.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)