Mh Waziri MKuu Akifanya mahojiano na Baraka Baraka
Urban Pulse Creative wakishirikiana na Star tv wanakuletea
Mahojiano Maalum na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofanya ziara
nchini Uingereza hivi karibuni. Mahojiano haya yalikuwa yamelenga zaidi
kupata ufahamu na uchambuzi wa namna serikali yetu ya Tanzania
inavyofanya kazi pamoja na changamoto zake.
Mbali na hapo tulijadiliana kuhusu Majukumu ya Waziri mkuu,
Chakula, Nishati, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mchakato wa katiba Mpya
kuelekea kuazimisha miaka 50 ya uhuru.
Mahojiano haya yalifanywa na Baraka Baraka Kutoka Urban Pulse na
yatarushwa Hewani kupitia kituo cha Star TV Jumapili ijayo Tarehe 30
octoba 2011 kuanzia saa 10.30 katika kipindi cha Medani za siasa.
Tafadhali usikose kuangalia kipindi hiki ili upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Tanzania na Serikali yetu.
Asanteni,
Urban Pulse Creative





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)