Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere akisalimiana na Waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe wakati alipotembelewa na ujumbe wa mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa kijijini kwake Butiama, mkoani Mara jana. Anaangalia kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mara, John Tupa na kutosho juu ni mtoto wa Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere
Mama Maria Nyerere( katikati) akiwa na Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini Balozi Juma wakiomba dua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kijijini Butiama wakati mabalozi hao walitembelea makazi na kaburi la Mwasisi huyo wa taifa la Tanzania. Wengine katika picha wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa, Waziri wa mambo ya nje, Bernard Membe wakati kwa upande wa kulia ni mwanae Charles Makongoro Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupa akitoa maelekezo kwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe wakati wa ziara ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa waliotembelea jana makazi na kaburi na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kijijini kwake Butiama mkoani Mara.
PICHA NA ANNA ITENDA- MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)