Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa
Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir
Safieldin.
Naibu
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw.
Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa
maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia
katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa
katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa
imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Mgeni rasmi akiongea na baadhi ya Wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma za Upimaji na Matibabu ya Masikio, Koo na Pua.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho hayo.
Meneja
Habari na Ushauri wa Taasisi ya John Hopkins Centre For Communication
Programme Tanzania Fauziyat Abood akitoa ufafanuzi wa Shughuli
zinazofanywa na Taasisi hiyo kwa mgeni rasmi alipotembelea katika banda
hilo.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)