Waziri
wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani akifafanua Jambo Mbele ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala mara baada ya
Kuwasilisha baadhi ya mabadiliko katika Muswada huo yaliyoletwa na
Serikali. Kamati hiyo ndiyo inayoshughulikia Muswada wa Mabadiliko ya
Katiba, kabla haujawasilishwa Bungeni.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema akifafanua mbele ya wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala baadhi ya vifungu
vilivyomo katika Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, ambao unashughulikiwa
na kamati hiyo kabla haujawasilishwa Bungeni. Waziri wa katiba na
Sheria Mhe. Celina Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliitwa
mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala Mhe.
Pindi Chana (Mb) akishauriana Jambo la kikanuni na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Mhe. Angela Kairuki (Mb), mara baada ya kupokea ufafanuzi wa
kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Kulia) na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema (hayupo Pichani) ambao
waliitwa mbele ya Kamati leo kufafanua baadhi ya vifungu katika muswada
wa Mabadiliko ya Katiba.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na
Utawala wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe.
Celina Kombani (Mb) aliyeitwa mbele ya kamati kutoa maelezo kuhusu
Maboresho katika Muswada wa Mabadiliko ya katiba. Kamati hiyo ha
Bunge iliwaita Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Celina Kombani (Mb) na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema kufafanua baadhi ya
vifungu katika muswada wa Mabadiliko ya Katiba.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)