Ndugu Watanzania Wenzangu
Kwa mara nyingine tena naomba tumshukuru
Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na uzima, na kunipa fursa ya
kuzungumza nanyi kwa kupitia utaratibu wetu huu mzuri wa kila mwisho wa
mwezi. Mwezi huu tunaoumaliza leo ulijawa na mchanganyiko wa mambo,
yalikuwepo mambo ya furaha na ya majonzi.
Tuliuanza mwezi kwa sherehe za Eid El-Fitr, kuadhimisha kumalizika kwa swaumu ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Nafurahi kwamba sherehe hizo zilifana na kuisha salama.Lakini, usiku wa tarehe 10 Septemba, 2011 katika mkondo wa bahari wa Nungwi, Zanzibar kulitokea ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander iliyokuwa na watu wengi na shehena kubwa ya mizigo. Mara baada ya taarifa ya ajali kutufikia hatua zilichukuliwa za kuokoa watu, meli na mali iliyokuwamo. Bahati nzuri ndugu zetu 619 waliweza kuokolewa wakiwa hai na sasa wanaendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa na kujiletea maendeleo yao. Maiti 203 waliweza kupatikana na kuzikwa kwa heshima. Maiti 197 walipatikana eneo la tukio, tano walipatikana Kenya na mmoja Tanga. Maiti waliopatikana eneo la tukio walizikwa Unguja na wale waliopatikana Kenya na Tanga walizikwa huko huko. Meli iliyozama haikuweza kuopolewa. Wataalamu wa uzamiaji wanasema ipo kwenye kina kirefu cha mita 300 ambacho hawakuweza kuifikia. Wao walifikia mita 58 tu. Wametushauri kuwa haitakuwa rahisi kuifikia meli hiyo, hivyo tukubali kuwa ndiyo makazi yake ya kudumu na vyote vilivyokuwamo ndani yake. Kwa kweli hatujui kwa uhakika kama wapo watu waliozama pamoja na meli hiyo au hapana. Bahati mbaya idadi kamili ya watu waliokuwamo katika meli hiyo haijulikani kwa uhakika. Orodha rasmi ya wenye meli inaonesha idadi ya watu waliokuwemo kwenye meli wakati inaondoka bandari ya Malindi, Zanzibar kuwa
pungufu kuliko idadi ya watu waliookolewa na maiti waliopatikana. Kwa sababu hiyo, huenda wapo watu waliozama na meli na kushindwa kutoka.
Ndugu Wananchi;
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amekwishaunda Tume ya Uchunguzi ambayo baada ya kumaliza kazi yake ndipo undani kuhusu ajali hiyo utapoweza kujulikana. Tume hiyo imekwishaanza kazi na kama kila kitu kitaenda kama ilivyopangwa, baada ya mwezi mmoja wataimaliza kazi hiyo. Napenda kutumia fursa hii kuwaomba watu mwenye taarifa zinazoweza kufanikisha kazi ya Tume hiyo wafanye hivyo.
Kwa mara nyingine tena narudia kutoa mkono wa pole na rambirambi kwa ndugu zetu waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali ile. Nawaomba waendelee kuwa na moyo wa subira na sisi wengine tujumuike nao kuwaombea marehemu wapate mapumziko mema. Kwa walionusurika tunaendelea kuwapa pole na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwaponya.
Ndugu Wananchi;
Narudia kutoa pongezi maalum kwa vyombo vyetu vya usalama na wale wote walioshiriki kuokoa maisha ya ndugu zetu waliozama na kuwaopoa maiti. Natoa pongezi za pekee kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na Makamu wake wawili kwa uongozi wao thabiti. Aidha, nawapongeza sana viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na wananchi wa Zanzibar kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya tangu kutokea kwa ajali, jitihada za uokoaji, maiti kuzikwa, majeruhi kutibiwa na kurejea makwao na kuwafariji wafiwa na walionusurika.
Mwisho, lakini siyo mwisho kwa umuhimu, nawapongeza sana wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kwa moyo wao wa upendo, ustahamilivu na mshikamano waliouonesha katika maafa haya ya kitaifa.
Safari ya Marekani
Ndugu Wananchi;
Kati ya tarehe 16 na 23 Septemba, 2011 nilifanya ziara ya kikazi nchini Marekani. Nilikwenda kuhudhuria Kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na shughuli zake. Pamoja na hayo nimehudhuria mikutano mingine kama vile Mkutano wa Open Government, ulioitishwa na Rais Barrack Obama wa Marekani,Mkutano wa Umoja wa Marais wa Afrika wa kupambana na malaria ,Mkutano wa Tatu wa Watanzania Waishio Marekani (DICOTA 3) na mkutano kuhusu Wanawake na Lishe ulioandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mama Hilary Clinton. Aidha, mimi na Waziri Mkuu, Stephem Harper wa Canada tulipata nafasi ya kuwasilisha taarifa ya Tume ya Afya ya Mama na Mtoto aliyoiunda Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambayo tulikuwa Wenyeviti wenza. Nafurahi kwamba taarifa yetu imepokelewa vizuri na kuelezwa kuwa itakuwa msingi mzuri wa kutatua matatizo ya vifo vya kina mama na watoto duniani. BOFYA HAPA KUENDELEA

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)