HATIMAYE MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE AFUNGA KAMPENI ZA CHADEMA IGUNGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

HATIMAYE MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE AFUNGA KAMPENI ZA CHADEMA IGUNGA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwaongoza wakazi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake kuonyesha ishara ya kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wa mkutano wa kufunga kampeni, kwenye Uwanja wa Barafu jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Ismail Jussa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakijaribu kumdhibiti mgombea wa ubunge jimbo la Igunga wa chama hicho, Leopard Mahona, ambaye alitaka kupigana na wafuasi wa Chadema, kutokana na kuingilia kwa mkutano wa Chadema katika kijiji cha Nyandekwa jana.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakijaribu kumdhibiti mgombea wa ubunge wa jimbo la Igunga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Leopard Mahona, ambaye alitaka kupigana wa wafuasi na viongozi wa Chadema kutokana na CUF kuingilia mkutano katika kijiji cha Nyandekwa jana.
Wananchi na Wanachama Wa Chadema Wakiangalia Chopa iliyokuwa ikitumiwa na Chadema katika kampeni ikiacha ardhi ya igunga tayari kwa wananchi kuingia katika zoezi la kupiga hapo kesho 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages