DEREVA
wa Roli aliyesababisha vifo vya watu 14 katika ajali iliyotokea eneo la
Msangamwelu Wilayani Chunya hivi karibuni, Moses Kapus (55) amesomewa
mashitaka 44 akiwa chini ya ulinzi katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea septemba 24 mwaka huu majira ya usiku baada ya roli aina ya fuso lililokuwa likitokea mnadani eneo la Mbuyuni wilayani Chunya kushindwa kupanda mlima na kuanguka .
Akimsomea mashtaka hayo mbele hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wa Wilaya, Michael Mteite, Wakili wa Serikali, Griffin Mwakapeje, alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa 44.
Mwakapeje alidai kuwa mshtakiwa, Kapus akiwa kama dereva alisababisha ajali kwa uzembe kutokana na kuendesha kwa kasi na kusababisha vifo vya watu 14.

Wakili
huyo alidai kuwa dereva huyo akiwa na gari aina ya fuso zenye namba
T582 AJF aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kusababisha majeruhi
43 ambao mpaka sasa hali zao ni mbaya na kwamba mshtakiwa huyo alitumia
gari hilo kinyume na aliyopewa .
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Mteite alisema mahakama imepokea makosa yote aliyosomewa mshitakiwa 44 .
Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Mteite alisema mahakama imepokea makosa yote aliyosomewa mshitakiwa 44 .
Hata hivyo mshitakiwa aliomba mahakama impe dhamana kutokana na hali yake kuwa mbaya kiafya, ambapo hata hivyo wakili wa serikali alimwomba Hakimu wa mahakama kuwa masharti ya dhamana yaangaliwe kwanza na yawe magumu kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya.
Aidha Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa kuwa na fedha taslimu sh. Milion 5 na wadhamini wawili wenye nyumba ili aweze kupata dhamana.
Hata hivyo Wakili wa serikali alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuwa tarehe ya shauri hilo itakuwa Octobar mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)