KOCHA
Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22
kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad
itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.
Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam
huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa
ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas
Ulimwengu.
Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam).
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab
(Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey
Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).
Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga),
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam),
Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver
Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An,
Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa
Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo- DRC).
Timu itaingia kambini Novemba 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na
inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena kwa
ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zitarudiana Novemba 15 mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)