WAKAZI WA MBUGA YA LOLIONDO WAGOMA KUMPISHA MWEKEZAJI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAKAZI WA MBUGA YA LOLIONDO WAGOMA KUMPISHA MWEKEZAJI

SAKATA la mgogoro wa ardhi dhidi ya mwekezaji katika mbuga ya Loliondo na wakazi wa Mkoani Arusha umeingia katika sura mpya baada ya Wakazi wake kugoma kuondoka katika eneo hilo kwa madai kuwa ni mali yao.

Wakizungumza katika tamasha la jinsia linaloendlea katika viwanja vyaTGNP jijini Dar es Salaam, wawakilishi wa wananchi wa Loliondo, walisema kuwa kwa pamoja wamekubalina kuwa hakuna mwananchi  atakayeondoka katika ardhi hiyo na kwamba serikali haijawatendea haki katika utatuzi wa mgogoro huo.

Walisema kuwa serikali ilibadilisha matumizi ya ardhi hiyo bila kuwashirikisha wananchi hao na kudai kuwa kulifanyika ukiuakaji wa haki za binadamu ambapo wananchi waliondolewa kwa kutumia nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na kuchomewa moto nyumba na mali zao.

“Tunaamini kuwa zoezi la kutuondoa katika eneo lile lilifadhiliwa na mwekezaji aliyewekwa na serikali bila kutushirikisha”alisema

mwakilishi mmoja wa wakazi wa Loliondoa aliyejitambulisha kwa jina la Kijoolu Kakeya, alisema kuwa katika sakata hilo serikali iliweza kutuma tume nyingi kwa ajili ya kufuatilia ukiukaji wa haki za binadamu ambazo hata hivyo hakuna hata tume moja mbayo imeweza kutoa majibu na yakawekwa wazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Arash Kiaro Orminis, alisema kuwa viongozi wa serikali walitumia madaraka vibaya ambpo waliwatimu wananchi na wengine kupigwa na kusababisha mtoto mmoja kupotea ambaye hadi leo hajapatikana haijachukuliwa hatua yoyote.

Alisema kuwa katika hekaheka hizo za kufukuzwa wananchi walipoteza mali zao nyingi na kwamba hadi sasa hakuna chochote katika suala hilo na hivyo kuwasabaishia wananchi hao usumbufu mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages