USIKU WA REDDS NIGHT OF FASHION WAFANA USIKU HUU KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

USIKU WA REDDS NIGHT OF FASHION WAFANA USIKU HUU KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE

Haya ni moja ya mavazi yaliowahi kuvaliwa na wasichana warembo katika miaka ya 1960, mavazi haya ni miongoni mwa mavazi yaliyotia fora katika onyesho la mavazi la Redds Night of Fashion linalofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, lengo la onyesho hilo ni kuwapa ubunifu na kuzindua vipaji mbalimbali vya warembo hao katika jumba la Vodacom House ili kuibua vipaji vyao vilivyojificha. Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Tanzania kwa muda mrefu sasa.
Momoja wa warembo akipita jukwaani na vazi lililowahi kuvaliwa katika miaka ya 1960 na wasichana warembo wa miaka hiyo.
Warembo wakipita na vazi la utambulisho jukwaani kama wanavyoonekana.
Wadau mbalimbali wa urembo wakifurahia jambo katika onyesho la mavazi la Redds Night Of Fashion.
Meneja wa Mwasiliano na habari za Mtandao Vodacom Tanzania Matina Nkurlu katikati akiwa na vimwana, waliowahi kufanya vyema katika mashindano ya Vodacom Miss Tanzania mwaka jana kulia ni Salma Mwakalukwa na kushoto ni Consolata Lukosi. Habari Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages