Ali Mango akiwa katika picha ya wimba ndani
ya Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alisema vazi hili ni maalumu
kwa kucheza na Nyoka.
Ali Mango ambaye pia
ni mtaalamu wa kucheza na nyoka kama tujuavyo Wanyamwezi na Wasukuma
katika ngoma xzao lazima kitu cha Chato lazima kiwakilishe na ngoma
inoge lazima kiwepo.
Ali Mango ni mmmoja kati ya wasanii
waliopata udhamini na Ubalozi wa Marekani ambaye atakuwa miongoni mwa
waasisis na wasanii watakaounda beni itakayokuwa na vionjo vya asili ya
makabila ya Kanda ya Ziwa yaani Wasukuma na Wanyamwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions ,
Amon Mkoga. http://www.chief/
promotions .or.tz 0755638004/0655638004.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakipata
ufafanuzi wa jambo fulani kutoka kwa Ali Mango MAELEZO, Dar es Salaam
leo asubuhi.
Amon Mkoga akionyesha kijarida kilichokuwa
na matukio ya tamasha la Mtemi Milambo lililofanyika Julai mwaka huu
mkoani Tabora.
WASANII wa Muziki
wa saili walioshiriki katika Tamasha la tatu la la Mtemi Milambo
mwaka huu lililofanyika Julai 8-10, 2011 katika viwanja vya Shule ya
Sekondari ya Uyui Mkoani Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa kwa wakati huo Mh. Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa
kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila makuu katika Kanda ya
Ziwa ambayo Wasukuma na Wanyamwezi wanaopatikana katika Mikoa ya
Tabora, Shinyanga na Mwanza.
Akizunguma katika Mkutano na
waandihi wa habari uliofanyika leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutano
Idara ya Habari (MAELEZO), Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions Amon
Mkoga alisema wasanii waliofanya vizuri mwaka huu ni Ali Mango ,
Asha Kaombwe, Hamisi Mpiga, Paulina Muhala na Paul Magadala.
Wsanii hao wataungana na wasanii
wengine wa miaka miwili iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa
asili itakayoitwa MWANAMILAMBO ambayo itakuwa ikipiga muziki wake
katika asili ya makabila hayo na utakuwa muziki wa hotelini , maharusi
na kumbi mbalimbali za burudani.
Mkoga
anazitaja nyimbo zitakazorekodiwa kuwa ni Kamnyangala Kane, Usoga wi
kuwa, Kushoke Kukaya, Kana nabuta, Sensema Malunde, Ng'ombe Yalala,
Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka 50 ya Uhuru.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa bendi hiyo ni
kusaidia kuhifadhi nyimbo mbalimbali za asili zilizotumiwa na wazee
wa kale katika vita, kilimo,harusi na hata mazishi.
"Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu
mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajili ya faida ya kizazi
cha sasa na kijacho" anasema Mkoga.
Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika Studio ya Aegies
chini ya muandaaji maarufu Peter John .a.k.a Nice P.
Pia kopi kadhaa zitatolewa latika vyuo,
makumbumbusho ya taifa na mashuleni ili wanafunzi na wanvyuo waweze
kuutambua utamaduni wao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)