Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akitoa salamu
zake za pole mara baada ya kumalizikia kwa dua ya pamoja iliyokuwa
maalumu kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli iliyotokea
Unguja Mwishoni Mwawiki
Katibu Mkuu kiongozi Philemon Luhanjo akitoa
tamko la serikali kuhusiana na ajali ya meli ya Spice Islander
iliyotokea mwishoni Mwawiki
Viongozi
mbali mbali walijumuika kwa pamoja na wananchi katika kuwaombea dua
wananchi waliofariki katika ajali ya kuzama meli ya Mv Spice Islander
katika maeneo ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja juzi,sla ya kuwaombea
dua maalum iliswaliwa katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar jana.
Baadhi ya
wananchi walioshiki katika sala na dua maalum wakiwa katika sala ya
maiti ya kuwaombe wananchi waliofariki katika ajali ya meli ya mv
Spice Islander katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar jana
Maelfu ya
wananchi wakimsikiliza Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi akiwahutubia wakati wa dua maalum ya kuwaombea katika
viwanja vya maisara Mjini Zanzibar.Picha na
Ramadhan Othman na Freddy Maro-IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk
Jakaya Mrisho kikwete akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,wakati wa Dua maalum ya
kuwaombea wananchi waliofariki katika ajali ya Meli ya Mv Spice
Islander katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)