Muasisi
na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima (kushoto)
akimkabidhi mfano wa hundi wa shillingi milioni 10 Makamu wa Pili wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kama rambi
rambi kwa familia za wafiwa na waliookolewa katika ajali ya meli
iliyotokea Zanzibar mapema mwezi huu.
Muasisi
na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima akiwa katika
mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea ofisi za Makamu wa Rais huyo asubuhi
ya leo (jana).
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Iddi
(watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka
Precision Air. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa Mauzo Zanzibar Laurian
Joseph, Afisa Mawasiliano Amani Nkurlu, Meneja Mauzo wa Zanzibar na Dsm
Nancy Bagaka, Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi Michael Shirima, Mkurugenzi
wa Biashara Phil Mwakitawa na Meneja wa Uwanja wa Ndege kwa Precision
Air Michael Montana.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)