Mgeni
rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea katikamahafali(kulia) ni
Mwenyekiti waJOHA TRUST Solomon Odunga katika maadhimisho ya miaka 11
ya shule Mfano ya sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson ,pamoja na
Mahafali ya 9 ya kidato cha IIV na Mahafali ya 6 ya kidato cha
VI.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete
akimkabidhi cheti mmoja ya kati ya wanafunzi wa shule ya mfano ya
Sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson(Sept,25,2011) jijini Dar es
Salaam wakati wa mahafali ya 9ya kidato cha IV na mahafali ya 6 ya
kidato cha IV pamoja na maadhimisho ya sherehe ya11 ya shule ya mfano.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete
akimpongeza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa
Muleba Kusini na Mwenyeliti wa Mwanzilishi wa JOHA TRUST Prof. Anna
Tibaijuka Sept 25,2011 huku Luguruni jijini Dar es Salaam katiak
maadhimisho ya miaka 11 ya shule Mfano ya sekondari ya Wasichana ya
Barbro Johansson ,pamoja na Mahafali ya9 ya kidato cha IIV na Mahafali
ya 6 ya kidato cha VI.
Na Anna Nkinda – Maelezo
Wito
huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Kikwete wakati akiongea na
wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Barbro Johansson iliyopo
Luguruni jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali ya kidato cha nne na cha sita.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwaambia wanafunzi hao kuwa elimu wanayoipata itafungua maisha yao na ya jamii nzima. Itawapa njia ya kuwa na uwezo kiuchumi, itawajengea uwezo wa kujiamini na kuweza kupaza sauti zao na kusikika kwani watakuwa na upeo mkubwa wa kuchambua mambo na kutoa maamuzi ya busara katika maisha.
“Ninafahamu
kwamba walimu, wazazi na walezi wamekuwa wakiwausia na kuwapa miongozo
katika maisha yenu ya kutafuta elimu. Jambo ambalo ningependa
muendelee kulizingatia kwa makini ni kwamba elimu mliyoipata bado ni
mwanzo tu, hasa ukizingatia kukua kwa utandawazi.
Siku
hizi mabadiliko ni ya haraka mno na yanamgusa kila mtu katika kila
nyanja ya maisha. Ni vizuri mkajua kwamba ni wajibu wenu kuendelea
kujifunza mbinu mpya za kuyakabili mabadiliko haya”, alisema Mama
Kikwete.
Mwenyekiti huyo wa WAMA alimalizia kwa kuwataka wanafunzi hao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwani elimu waliyonayo haitakuwa
na maana kama wataruhusu kuambukizwa ugonjwa huo na kupata ujauzito
ambao utawafanya wakatize masomo yao na hivyo kutotimiza ndoto zao.
Akisoma taarifa ya shule hiyo Mkuu wa Shule Halima Kamote alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo miaka 11 iliyopita jumla
ya wahitimu 471 wa kidato cha nne na 282 wa kidato cha sita walihitimu
masomo yao na kufaulu kwa kiwango cha juu na kufanikiwa kujiunga na
vyuo mbalimbali na vya elimu ya juu hapa nchini.
Kamote alisema , “Katika mahafali ya leo tunao wahitimu 76 wa kidato cha nne na 151 wa kidato cha sita ambao tunaamini kutokana na elimu waliyoipata
kutoka kwa walimu wao watafanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa
na hivyo kuendelea kutunza heshima ya shule yetu katika jamii”.
Shule hiyo yenye wanafunzi
632 wa kidato cha kwanza hadi cha sita, walimu 37 na wafanyakazi
wengine 27 imekuwa ikipata msaada kutoka Serikali ya Sweden kupitia
ubalozi wake hapa nchini ambao umetumika kujenga majengo, matanki ya kuhifadhi maji na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wenye vipaji kilaaluma ambao wanatoka katika familia zenye kipato duni.
Alizitaja
changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni upungufu wa majengo, wafadhili
wakuu wa shule hiyo ambao ni SIDA wanatarajia kukatisha ufadhili wao
mwishoni mwa mwaka huu na hivyo kuzua tatizo la kukosekana kwa ufadhili
wa uhakika wa ada kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni.
“Changamoto
nyingine zinazotukabili ni wanafunzi wanaofadhiliwa na shule hii
wanakosa mikopo pale wanapojiunga na elimu ya juu pengine ni kwa kuwa
wanatoka katika shule binafsi ambako kuna ulipaji wa ada unaoendana na
gharama halisi na mahitaji ya kujiunga na shule ni makubwa kuliko uwezo wa shule”, alisema.
Kila
mwaka sherehe za mahafali ya shule hiyo hufanyika tarehe 25 Septemba
ili kuienzi siku aliyozaliwa Dk. Mama Barbro Johansson ambaye ni
mmisionari, mwalimu, mwanaharakati na mwanadiplomasia kutoka nchini
Sweden ambaye alitoa mchango mkubwa katika kupigania elimu ya watoto wa
kike na wa kiume.(Picha na Mwanakombo Jumaa_MAELEZO)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)