MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AUNGURUMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA IDARA YA SAYANSI ZA KIMATAIFA SWEDEN - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AUNGURUMA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA IDARA YA SAYANSI ZA KIMATAIFA SWEDEN

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa mhadhara na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali zilizopo chuoni hapo jana Sept. 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Uppsala Sweden, Bo Sundavist (katikati) na Mkurugenzi, Romain Murenzi, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ua Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo nchini Sweden. Mhadhara wa maadhimisho hayo ulifanyika jana Sept. 26 nchini hapa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Prof. Mohamed Hassan (kushoto) Prof. Jean-Piere Ezin (wapili kushoto) na Prof. Mohamed Elton, baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden, jana Sept. 26.
MamaAsha Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Chuo cha Uppsala, Mikael Norrby, kuhusu Viumbe vilivyokaushwa na  kuhifadhiwa  katika Jumba la makumbusho la Gustavo Adolpho nchini Sweden, wakati Mama Asha alipotembelea katika Jumba hilo na kujionea mambo mbalimbali ya kisayansi yaliyomo katika Jumba hilo jana sept. 26. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages