Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa
Pencheni ya mashirika na taasisi za umma Bw, William Erio akimkabidhi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hundi ya Sh,
Milioni kumi kusaidia mfuko wa maafa wa Zanzibar kufuatia ajari ya meli
ya Mv. Spice Islanders iliotokea hivi karibuni
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifafanua jambo mara
baada ya kupokea hundi ya sh, milioni kumi kutoka kwa uongozi wa mfuko
wa pencheni ya mashirika na taasisi za umma PPF kusaidia mfuko wa maafa
wa Zanzibar kufuatia ajali ya mv spice. Pichani kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa PPF Bw William Erio akiwa na ofisa uhusiano wake Bibi Lulu
Mengele
----
Na Othman Khamis
Ame
Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amepokea ubani kutoka kwa Uongozi
wa Mfuko wa Pencheni ya Mashirika na Taasisi za Umma Tanzania {PPF }
ili kufariji watu waliopatwa na maafa ya kuzama na Meli ya M.V Spice
Islanders.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF Bwana William Erio alimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hundi ya Jumla ya shilingi milioni kumi
Kusaidia mfuko wa Maafa Zanzibar unaoratibu shughuli zote za Maafa
Zanzibar.
Bwana
William amesema Maafa yaliyowapata wananchi hao yamegusa Taasisi yao
na Jamii yote ya Watanzania. Amewataka waliokumbwa na Mtihani huo kuwa
na subira katika kipindi hichi kigumu cha Janga hilo.
Akipokea msaada huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Balozi Seif Ali Iddi
amezipongeza Taasisi na Jumuiya zote ndani na nje ya Nchi zinazoendelea
kutoa misaada yao.
Balozi Seif amesema misaada inayoendelea
kutolewa inaashiria mshikamano uliopo kati ya Serikali, Taasisi tofauti
pamoja na Wananchi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)