Mkufunzi kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu Bi. Neema Ngure akitoa ufafanuzi wa fomu
za dodoso zitakazotumika kwenye sensa ya majaribio ya watu na makazi
2011 kwa wafanyakazi watakaosimamia zoezi hilo litakalofanyika mwezi
ujao katika maeneo mbalimbali nchini wakati wa semina ya mafunzo leo
mjini Morogoro.
Wafanyakazi watakaosimamia zoezi la sensa ya majaribio ya watu na makazi 2011 kutoka maeneo mbalimbali nchini
wakifanya mtihani wa kupima uelewa leo mjini Morogoro wakati wa semina
ya mafunzo ya usimamizi wa zoezi la sensa litakalohusisha maeneo ya
mikoa ya Dar es salaam, Kanda ya ziwa, Kanda ya kati, mikoa ya kusini
na nyanda za juu kusini pamoja na Zanzibar. 





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)