Wasanii wa kundi la mutati wakilakiwa na mwenyeji wao kutoka Kampuni ya Shear Illusions Dora Raymond .
Wasanii
wa miondoko ya Salsa wa kundi la Mutati la nchini Kenya wakiwasili leo
jioni katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, wasanii
hao wataburudisha katika hafla ya Shear Ball itakayofanyika Jumamosi
katika Hoteli ya Movenpick.
Hafla
hiyo inalenga kuchangisha milioni 50 za kusaidia ukarabati wa mfumo wa
maji taka katika hospitali ya Mwananyamala pamoja na kusaidia fedha za
matibabu kwa wanawake wenye kuugua ugonjwa wa fistula.
Wasanii hao wanne ni Yassin Mutati aliyevaa njano, Triza Wanjeri, Alice Kang'ara na Daniel Mutema.
Wakielekea vyumbani kupumzika mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Peacock ambayo ni mmoja kati ya wadhamini.
Wasanii
wa kundi la Mutati wakiwa katika picha ya pamoja na Head of Marketing
and Corporate Affairs Dorah Raymond (wa pili kushoto).









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)